Kuhusu Tezi Dume - Disease Details

Kuhusu Tezi Dume

Tezi dume (prostate) ni tezi ndogo inayopatikana kwa wanaume pekee, ipo chini ya kibofu cha mkojo na inazunguka sehemu ya mwanzo ya mrija wa mkojo. Kazi yake kuu ni kutengeneza na kutoa majimaji yanayolisha na kulinda mbegu za kiume wakati wa utoaji mbegu. Magonjwa yanayoipata mara nyingi ni kuongezeka kwa tezi dume kutokana na umri (BPH) linalosababisha kukojoa mara nyingi na mkojo kutotoka vizuri, uvimbe au maambukizi ya tezi dume (prostatitis) yanayoleta maumivu na homa, pamoja na kansa ya tezi dume ambayo hutokea zaidi kwa wanaume wenye miaka 50 na kuendelea.

Posted on: 2025-11-14 02:37:49

Request Medicine
Dr Mbilinyi - Footer Example