Mahusiano sumu yana mchango mkubwa katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa sababu mazingira ya msongo wa mawazo, migogoro ya mara kwa mara na ukosefu wa amani huathiri moja kwa moja homoni na mfumo wa damu wa mwanaume. Wakati mwanaume anaishi kwenye toxic relationship, mwili huzalisha kiwango kikubwa cha homoni ya stress (cortisol), ambayo inapoongezeka hupunguza uzalishaji wa homoni muhimu ya kiume, yaani testosterone. Kupungua kwa testosterone kunasababisha kushuka kwa hamu ya tendo la ndoa, uume kushindwa kusimama kikamilifu, uume kusinyaa katikati ya tendo pamoja na kuwahi kumwaga. Zaidi ya hapo, ugomvi wa mara kwa mara na maneno ya kudhalilisha hupunguza kujiamini, hali inayoupeleka ubongo kwenye ‘fight or flight mode’ na kuzuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume, hivyo kusababisha nguvu za kiume kudhoofika. Katika mahusiano yenye wivu, lawama na presha ya ku-perform, mwanaume hutengeneza hofu ya kushindwa, ambayo pia huathiri uwezo wa mwili kujibu vizuri wakati wa tendo la ndoa. Hii inaonyesha kuwa tatizo la nguvu za kiume si la mwili pekee, bali pia hutokana na mazingira ya kihisia anayopitia mwanaume kila siku. Kwa hiyo, ili kurejesha nguvu za kiume, ni muhimu kutengeneza amani ya ndani, kupunguza msongo wa mawazo na kuepuka mahusiano yenye sumu ambayo yanaharibu afya ya uzazi bila mwanaume kujua. — Dr. Mbilinyi
Posted on: 2025-11-16 22:25:21
Request Medicine