Saratani ya tezi dume huanza kimya kimya bila maumivu, ndiyo maana wanaume wengi huigundua wakiwa kwenye hatua za mbele. Lakini zipo dalili muhimu ambazo ukiziona, unapaswa kuchukua hatua mapema.
1. Kujisikia Mkojo Hauishi (Incomplete Emptying)
Unakojoa lakini bado unahisi kibofu hakijaisha au unataka kurudi tena baada ya muda mfupi.
2. Kukojoa Mara Kwa Mara Sana
Hasa usiku—unashindwa kulala kwa sababu ya kwenda chooni mara nyingi.
---
3. Maumivu au Kuchoma Wakati wa Kukojoa
Hii inaweza kuashiria kuwa tezi dume imevimba au inakandamiza njia ya mko
4. Mkojo Kutoka Kwa Nguvu Ndogo
Mkojo kutoka kwa drip, kuvutika, au kukatika katikati. Hii ni dalili muhimu ya shinikizo kwenye urethra.
---
5. Damu Katika Mkojo au Shahawa
Hii ni ishara kubwa inayohitaji uchunguzi wa haraka
6. Maumivu Sehemu ya Chini ya Mgongo, Hips au Mapaja ya Juu
Inapotokea saratani imeanza kusambaa (metastasis), huleta maumivu ya mifupa upande wa chini ya mgongo na nyonga
7. Kupungua kwa Nguvu za Kiume (Erectile Dysfunction)
Si mara zote, lakini saratani ya tezi dume inaweza kuathiri mishipa na kusababisha uume kushindwa simama ipasavyo.
8. Kushindwa Kudhibiti Mkojo
Unaanza kupata leakage au kushindwa kuzuia mkojo vizuri.
9. Maumivu Wakati wa Kumwaga (Ejaculation Pain)
Hii inaweza kuashiria uvimbe kwenye tezi dume.
DALILI ZA HATUA ZA MBELE (Advanced Stage)
Ikiwa saratani imeenea zaidi:
Uchovu uliokithiri
Kupungua uzito bila sababu
Miguu kuvimba
Maumivu ya mifupa yanayoongezeka
MUHIMU KUFAMU:
Saratani ya tezi dume huonekana zaidi kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 40–70, wachuuzi wa bidhaa za kemikali, walioshindwa kupunguza msongo wa mawazo, na wale wenye historia ya familia.
Uchunguzi wa PSA na Digital Rectal Exam (DRE) ndiyo njia sahihi kugundua mapema.
Posted on: 2025-11-22 16:01:09
Request Medicine